Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Utawala wa kigaidi wa Kizayuni ulizidisha mashambulizi yake ya kinyama katika baadhi ya makazi ya raia wa Mji wa Tehran alasiri ya leo Jumapili ya tarehe 15 Juni.
Eneo la Hemmat Highway, eneo la Valiasr Square, eneo la Niavaran, na Mtaa wa Sohrudi ni miongoni mwa maeneo ambayo yamelengwa katika saa chache zilizopita.
Katika mashambulizi hayo ya kiupofu na ya kikatili, baadhi ya majengo ya makazi yalilengwa na baadhi ya wananchi wakiwemo wanawake na watoto kujeruhiwa. Jana usiku, jengo la makazi katika kitongoji cha Narmak mashariki mwa Tehran lilipigwa makombora ya utawala wa Kizayuni unaoua watoto na wanawake.
Your Comment